Wednesday, November 16, 2016

Matteo Darmian haelewi kwanini mpaka sasa kocha Jose Mourinho amekuwa hana imani naye na kumpa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Kwa sasa Darmian amekuwa mnufaika wa majeruhi Antonio Valencia, Luke Shaw na Chris Smalling, hivyo kupata nafasi ya kucheza baada ya kukosekana kwa wachezaji hao.

Kukosekana kwa Valencia ambaye anauguza jeraha la mkono, Darmian atakuwa na nafasi ya kuanza katika mchezo wa Premier League dhidi ya Arsenal utakaochezwa Jumamosi ya wikiendi hii kunako Uwanja wa Old Trafford.

Alipoambiwa azungumze kwanini amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza, Darmian alijibu: "Sijui kwanini, hilo ni swali gumu sana kwangu kujibu. 

"Kocha ndiyo mtu pekee mwenye maamuzi ya kupanga wachezaji na jukumu letu sisi wahezaji ni kukubaliana naye tu. Mara nyingi nimekuwa nikijituma sana na nitaendelea kufanya hivyo.

"Kimsingi sijapoteza mtazamo wangu chanya, hasa katika kipindi ambacho nimekuwa sipati nafasi kubwa ya kucheza. 

"Kuanzia siku ya kwanza kabisa nimekuwa nikijitahidi kuonesha ubora wangu kwa kocha."

Alipoulizwa juu ya ripoti za kujiunga na Inter, Darmian amesema: "Sijui, ni mapema mno kuzungumzia juu ya masuala ya usajili. Kesho nitarejea klabuni Manchester na tunakabiliwa na mchezo muhimu sana dhidi ya Arsenal, ambapo kila mmoja anataka kucheza."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video