Sunday, November 6, 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo kwa timu kuchuana kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, African Lyon inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo Na. 144, wakati Mbao itakuwa mwenyeji wa Azam FC Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mchezo Na. 116.

Kwa upande wake, Ndanda watakuwa wenyeji wa Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kwenye mchezo Na 117, wakati Tanzania Prisons inatarajiwa kuialika Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo Na. 118.

Kagera Sugar kwa upande wake itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mchezo ulipewa Na. 119, ilhali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani kwenye mchezo Na. 120.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar itaialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Morogoro katika mchezo Na. 113 wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga katika mchezo ulipewa Na. 115.

KIFUPI

RATIBA YA MECHI ZA LEO LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA
African Lyon vs Simba SC (Live Azam Sports HD)
Tanzania Prisons vs Yanga SC (Live Azam TWO)
Mbao FC vs Azam FC ( Live Azam ONE)

MECHI NYINGINE

Ndanda FC vs Stand United
Kagera Sugar vs Ruvu Shooting
JKT Ruvu vs African Lyon

VPL JUMATATU (NOVEMBA 7, 2016)
Mtibwa Sugar vs Mbeya City
Mwadui FC vs Majimaji FC

@@@@MPENJA SPORTS

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video