Tuesday, November 1, 2016

Ligi ya Kuu ya Wanawake Tanzania imeanza leo kwa viwanja vitano kutimua vumbi nchini, huku timu ya JKT Queens ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mlandizi Queens.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume, JKT Queens walijpatia bao la kwanza kupitia kwa Donisia Minja dakika ya 10 ya mchezo, kabla ya Mwanahamis Omary kuisawazishia Mlandizi Queens dakika ya 12.

Fatuma Mustapha aliifungia JKT Queens mabao mawili dakika ya 16 na 77 kabla ya Mwanahamis Shurua kuhitimisha kalamu ya mabao dakika ya 80. Ligi hiyo ya Wanawake inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini wenye makundi mawili, huku ikiwa ni kwa mara ya kwanza kabisa Tanzania kuwa na Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake.

Matokeo mengine:

Viva 1-1 Mburahati

Fair Play 0-2 Evergreen

JKT queens 4-1 Mlandizi

Marsh 5-0 Majengo

Baobab 0-0 Kagera

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video