Sunday, November 6, 2016

Mara nyingi Yanga imekuwa ikitumia mfumo wa 4-4-2 kwa tactical patterns za kuua wings na mashambulizi ya upande yakianzishwa na full backs ambao hucheza kama wing backs.

Leo anakuja na deception plan ya 4-3-3 ndani ya 4-4-2 kwa aina ya wachezaji aliowapanga kwenye wings na forwad line. 

Tukianzia kwenye backline, Tambwe kiasilia ni kiungo mkabaji lakini kiraka na ana uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi . Kumwanzisha beki namba mbili na ukiangalia beki huyo si mzuri kupanda hii ina maana Pluijm hatakwenda na mfumo wake wa siku zote mabeki kupanda bali watafanya marking chini ya mstari wa kati . Watapanda juu kwenye pressing tu ikihitajika . 

Hii ni dhahiri chini kutakuwa na watu 4 ambao juu yao kutakuwa na viungo watatu. Wawili wakabaji na mmoja mshambuliaji kificho pembeni au play maker wa pembeni ambaye huyu ni Yusufu Mhilu. Kaseke atamzunguka Kamusoko kumpa back ya marking lakini pia atasogea juu kutengeneza mashambulizi ya pembeni chini ya Obrey Chirwa ambaye ni second striker kwa Donald Ngoma. 

Ngoma , Chirwa na Kaseke wote hawa ni false 10 ambao nyuma yao yupo Haruna Niyonzima kama mpishi wa juu. 

Sasa kwanini nilisema kuna uwezekano mkubwa wa Pluijm kucheza 4-3-3?! msingi mkubwa wa mfumo wa 4-3-3 nikuwa na attacking midfielder kiasilia zaidi ya mmoja . Ngoma , Chirwa, Mhilu na Deusi Kaseke wote hawa kimbinu ni attacking mids wenye uwezo mzuri kukaa na mpira , kukokota , kutoa pasi nzuri za mwisho na uwezo mzuri kupiga mashuti ndani ya 18 au nje ya 18. 

Alicholenga Hans ni mpira wa kasi wenye pasi nyingi ambao utatawaliwa na viungo na hii ni kutokana na makosa ya mechi iliyopita ambayo waliacha mchezo wao wa pasi za haraka kwenda mbele na kutumia long balls ambazo mara nyingi ni kamari kimbinu kwa kutafuta counter attack.

Samuel Samuel

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video