Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amefurahia sana maisha yake ya kudumu miaka yake 20 akiwa klabuni hapo, ikiwa ni pamoja na kuitawala na kuwa mbabe wa Tottenham ambao ni mahasimu wao wakubwa kwenye jiji la London.
Kwenye mechi 191 ambazo timu hizo zimekutana, Arsenal wameshinda mara 80, Spurs mara 61 na 50 zimemalizika kwa sare
Tangu awe meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amecheza michezo 48 ya Premier League dhidi ya Spurs na kushinda mara 22- sawa na uwiano wa asilimia 46, ametoka sare mara 19, kwa maana kwamba ameweza kujinyakulia pointi kwa asilimia 85 ya mechi dhidi ya mahasimu wao hao.
0 comments:
Post a Comment