Monday, November 7, 2016

Kwa niaba ya wachezaji, napenda kutoa au kuomba samahani kwa Wanasimba wote wanaojitolea kwa hali na mali kufanikisha au kutaka kuona timu au simba kiujumla inafanya vizuri.

Ila leo tumepoteza points 3 ambazo ni muhimu kwetu kama tulivyojiwekea malengo yetu ni kupata points 3 kwa kila mechi ili kufikia malengo yetu katika msimu huu.

Ila naomba au kutoa angalizo juu ya kupoteza mchezo wetu wa leo. Tunahitajika kuwa wamoja zaidi na kuangalia tatizo lilikuwa wapi turekebishe ili tuweze fikia malengo tuliyojiwekea. 

Ila tukichukua maneno ya wapinzani wetu tukachanganya na matokeo ya leo, tutazidi kuumia na kuchanganyana zaidi na kutoka kwenye mstari na kujiteketeza wenyewe na kuwapa nafasi watu wasiopenda kuona simba inafanya vizuri.

Poleni sana na poleni tukubali matokeo na tustuke kwa kila idara kama iliona tayari tumemaliza au tumepata. Basi tuamke na kuzidisha kufanya yale tuliyokuwa tunayafanya na kupata matokeo yatakayotufanya kufikia malengo. 

Mussa Hassani Mgosi,
Meneja wa timu ya Simba

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video