Sunday, November 6, 2016



Na Samuel Samuel
Mmoja kati ya wachezaji ambao watamkumbuka sana mzee Hans van der Pluijm katika kujenga na kukuza kipaji chake katika soka ni Saimoni Happygod Msuva winga wa kulia wa Yanga SC.
Hans Van hajawahi kumkatia tamaa mchezaji huyu ambaye kwa nyakati fulani alikuwa akiwakera sana mashabiki na wapenzi wa Yanga SC kwa aina ya uchezaji wake. Saimoni Msuva alikuwa akivunja mipango mingi ya timu hiyo kusaka magoli kwenye safu ya ushambuliaji kwa papara zake katika kufunga. Mara nyingi alikuwa akipoteza nafasi za wazi kwa kushindwa kuinua macho na kuwatizama wenzake wamejipanga vipi timu inapoingia kwenye eneo la adui.
Kasumba ya ili uwe bora kwenye timu ni lazima ufunge ilimtesa mchezaji huyu na kujikuta akivuruga mipango mingi inayosukwa vyema na wenzake toka nyuma . Sehemu ya kutoa pasi yeye alipiga shuti hata akiwa kwenye " impossible angle" hali iliyokuwa ikimfanya kuonekana kituko licha ya uwezo mkubwa alionao katika kukokota mipira kwa kasi na kuachia mashuti ya mbali.
Kelele za mashabiki za kumtaka anyimwe nafasi ya kikosi cha kwanza hazikumwingia akilini mwalimu Hans Van Pluijm zaidi ya kuzidi kumsuka kijana wake awe na utulivu katika eneo la mwisho la ushambuliaji kuzingatia misingi mama ya winga wa pembeni ambayo ni kuwachezesha washambuliaji wa kati au kuingia kwenye eneo la ulinzi la adui kwa kasi kabla ya safu ya ulinzi ya wapinzani haijajipanga na kufunga kwa mashuti makali ya pembeni ambayo mara nyingi ni low kick, volley na semi volley.
Msuva baada ya mafunzo , uvumilivu wake na kutambua thamani yake ndani ya kikosi cha Yanga , mwezi uliopita wa kumi amewatengenezea wenzake nafasi tano za kufunga , yeye mwenyewe akifunga magoli manne katika mechi 4 za mwezi Octoba.
Katika mwezi Octoba Yanga ilipata alama 9 na magoli 16 katika mechi nne na Saimoni Msuva katika magoli 16 ana mchango wa moja kwa moja katika magoli 9! . Manne akifunga mwenyewe na matano akitoa pasi nzuri za mwisho wenzake kufunga lakini pia akisimama imara kama injini ya mashambulizi ya upande kwa Yanga SC .
Uwezo wa kufikiria masilahi ya timu kiliko masilahi binafsi ndio vimenifanya niandike makala hii juu ya mchezaji huyu ambaye ameing'arisha vyema timu yake dhidi ya wapinzani.
Ubora wa Arsenal FC unategemea uimara wa Mesut Ozil ambaye ndie chanzo kikubwa cha magoli mengi ya klabu hiyo kwa pasi zake maridhawa. Licha ya hivi karibuni kuanza kutikisa nyavu lakini ubora na thamani yake ndani ya klabu hiyo kongwe nchini England ni pasi na krosi zake nzuri za mwisho " master of assist". Hiki ndicho Msuva anachokifanya sasa ndani ya Yanga SC. Anahitaji muda zaidi kudhirisha ubora wake kwa timu yake na timu ya taifa aliyopata kibali cha kuichezea kwa maendeleo yake mazuri.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video