Sunday, November 6, 2016

Simba SC waliingia mchezoni wakijiamini vyema dhidi ya African Lyon kwa mwendelezo mzuri wa matokeo ya nyuma.

Hesabu za Bernardo mreno wa African Lyon zilitofautiana na Joseph Omog kocha mkuu wa Simba SC . Bernado alijipanga kuzuia na kushambulia kwa kuvizia lakini mahesabu makubwa katika kuzuia aliwapanga vijana wake kukabia juu ya mstari na sio kupaki basi katika mfumo wao wa 4-4-1-1 waliokuwa wakiutumia lakini pia wakichanganya na 4-5-1 ili kuvunja maelewano ya viungo wa Simba SC pale kati. 

Omog kwa asilimia nyingi alijipanga kushambulia pande zote. Alimweka Mwinyi Kazimoto kushoto kama kiungo mchezeshaji wa pembeni pia kiungo mshambuliaji kificho akitumia 4-4-2. Kichuya kulia na Mzamiru Yassin kama mchezeshaji nyuma ya Mohamedi Ibrahimu . Wote hawa ni wana uwezo mzuri wa kukaa na mpira na kushambulia lakini ubora wao unategemea kiungo cha chini kimejipanga vipi pia wing backs wanasaidia vipi mashambulizi hayo. 

African Lyon walichofanya ni kuhakikisha Jonasi Mkude anakosa mawasiliano mazuri na Mzamiru Yassini ili kuvunja mawasiliano ya kati kwa kiungo na safu ya ushambuliaji . 

Walipokuwa wakipoteza mpira Lyon wananadilika kutoka 4-4-1-1 na kucheza 4-5-1 ili Kuziba njia za mpira na kupunguza eneo la kucheza kwa Simba SC kujipanga kwa mashambulizi. 

Lyon walidhamiria kuwakataa Simba SC kwenye kwenye pasi fupi fupi za haraka kuja langoni mwao ( direct play ) na kuwalazimisha wacheze sana kwenye eneo lao kwa squre passes na wakijaribu kusogea juu watumie mipira mirefu ambayo mara nyingi si mizuri kujenga mashambulizi. 

Mbinu hizi zilimfanya mshambuliaji wa Simba SC Laudit Mavugo kushindwa kupata mipira na muda mwingi kuwa off target mpaka alipotolewa na kuingia Saidi Ndemla. 

Mashambulizi ya kuvizia yaliwapa goli la jioni Lyon wakifanikiwa kwenye mbinu zao . Walilenga kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza lakini mfumo wao wa kujilinda ndio uliowafanya Simba SC kupotea uwanjani kwa kukabia juu. 

Samuel Samuel

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video