Saturday, November 5, 2016

Eden Hazard usiku wa leo amefunga mabao mawili na kuipeleka Chelsea kileleni mwa Premier League kwa mara ya kwanza tangu mwezi August baada ya kubamiza Everton mabao 5-0 kwenye Stamford Bridge.

Hazard alifungua milango ya mabao kwa Chelsea baada ya kufunga goli zuri kabisa la kuchungulia kabla ya beki wa kushoto wa timu hiyo Marcos Alonso kufunga la pili kwa kumpiga tobo kipa wa Everton Maarten Stekelenburg

Diego Costa alishindilia msumari wa tatu baada ya kupiga shuti kali kufuatia kona iliyochongwa na Pedro kabla ya kwenda mapumziko.

Pedro alifunga bao la nne baada ya kipa kuutema mpira kufuatia shuti kali lililopigwa na Eden Hazard na kumfikia hatimaye kuukwamisha kiulaini.

Everton walitumia muda mwingi kucheza katika eneo lao na kushindwa kupiga hata shuti moja lililolenga langono mwa Chelsea katika muda wote wa dakika tisini huku Chelsea wakiwashambulia mithili ya nyuki waliotibuliwa.

Matokeo mengine

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video