Wednesday, November 16, 2016

Mwenyekiti wa Kamati ya Usaji ya Simba Zacharia Hans Poppe amejinasibu kuwa msimu huu wamejipanga dhidi ya hujuma zote kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka wahakikishe kinaeleweka.

Hans Poppe amesema miaka mingi mingi wamekuwa wakijikwaa na kupuuza lakini safari hii wamejizatiti kwa umakini mkubwa mno.

"Kuna msemo unasema kwenda mjinga kurudi je...maana unaweza kuwa hujiui njia sasa wakati wa kurudi umeshajua kuna njia gani, kwa hiyo unakuwa unafahamu kuwa sehemu gani mwiba upo na sehemu gani hamna," amesema.

Amesitiza kuwa msimu huu ni wao hata iweje na wamejipanga kuhakikisha ubingwa unatua Msimbazi baada ya kuukosa kwa muda mrefu.

Amejisifu kwamba misimu mingi iliyopita mpaka muda huu wanakuwa hawapo kwenye nafasi nzuri, lakini kitendo cha kushika usukani msimu huu mpaka sasa kinaashiria namna gani walivyojipanga.

"Kwa vyovyote vile mpaka sasa umeona pamoja na mambo yote haya sisi tuko top (juu). Mwaka jana tulikwensa tukayumba yumba, tunatetereka na kushuka nafasi ya pili au ya tatu,lakini safari hii mashine inachanganya tu hata ufanya namna gani."

"Safari hii tumenuia kuchukua ubingwa na ndio tunaoutaka na hatusikii la mnadi swala wala la muadhini."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video