Tuesday, November 1, 2016

Jose Mourinho yuko mbioni kukabiliwa na adhabu nyingine tena kutoka Chama cha Soka England (FA) baada ya hapo awali kuondolewa kwenye benchi katika mchezo kati ya Manchester United na Burnley uliomalizika kwa suluhu.

Bosi huyo wa zamani wa Chelsea tayari ana adhabu iliyotokana na kutoa matamshi yasiyoridhisha juu ya mwamuzi Anthony Taylor wakati wa kuelekea mchezo kati ya United na Liverpool

Na sasa anaweza kukumbwa na adhabu ya kutohudhuria kabisa uwanjani kufuatia matamshi yake yasiyofaa dhidi ya mwamuzi Mark Clattenburg Jumapili iliyopita ambapo anatuhumiwa kwa kutoa maneno yaliyokuwa na matusi na kejeli ndani yake.

Mpaka Ijumaa saa mbili kamili usiku, Mourinho anatakiwa kuwa ameshajibu tuhuma hizo kabla ya kukabiliwa na adhabu hiyo.

Mara ya kwanza alipaswa kujibu tuhuma hizo jana Jumatatu lakini hata hivyo hakuwasilisha rufaa yoyote ile.

Mashtaka juu ya Mourinho yanaelezwa kutokana na kauli chafu alizotoa dhidi ya Clattenburg katika mchezo dhidi ya Burnley baada ya kudai mwamuzi huyo kuwanyima penati iliyotokana na Jon Flanagan kumkwatua Matteo Darmian ndani ya eneo la penati.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video