Saturday, November 12, 2016

Taarifa kwa vyombo vya habari;

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani, COREFA, imeusimamisha uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Rufiji (RUFA) uliokuwa umepangwa kufanyika Jumapili, Novemba 13, 2016 kwa kukiuka taratibu.

Taratibu zilizokiukwa ni pamoja na kutokuwepo kwa taarifa kuhusu mchakato wa uchaguzi huo, vyeti vya elimu vya wagombea kutohakikiwa Baraza la Mitihani (NECTA) na baadhi ya vilabu na vyama wanachama ambavyo havijafanya uchaguzi kuingizwa katika orodha ya wapiga kura.

Kamati ya Uchaguzi ya Mkoa, COREFA imeusimamisha uchaguzi huo hadi hapo taratibu zilizokiukwa zitakaporekebishwa ili viongozi watakaochaguliwa wawe wamekidhi sifa na vigezo kwa mujibu wa Katiba ya RUFA, COREFA na Kanuni za uchaguzi za TFF.

Kamati ya Uchaguzi ya Mkoa, COREFA imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUFA kuanza upya mchakato  huo wa uchaguzi mapema iwezekanavyo kwa kufuata maelekezo iliyowapa ili kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki, usio lalamikiwa kwa kuvunja Katiba na kutokufuata taratibu na kanuni za uchaguzi.

Imetolewa na,
Masau Bwire 
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi COREFA.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video