Tuesday, October 11, 2016



Na Abdallah Saleh-Mdau wa MPENJA SPORTS

Mchezo utakuwa na ushindani mkubwa kwa kuzingatia ubora wa vikosi vyote na nafasi katika msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Mtibwa Sugar inayoshika nafasi tatu ni wazi wataingia kwenye mchezo wakitaka kukusanya alama zote tatu ili kuendelea kujiweka mazingira mazuri zaidi.
Kwa upande wa Mabingwa Watetezi, Yanga,  bila shaka wataingia Uwnajani kusaka alama tatu muhimu ili kufufua matumaini ya kuutetea ubingwa wao ambao yameingia doa kwa kutoa sare mbili na kupoteza mechi moja kati ya mitanange sita walizocheza mpaka sasa, japokuwa kimpita bado ni mapema mno.
Kiufundi Mtibwa Sugar wanaonekana kuimarika sana kwa kiwango chao hasa katika michezo ya hivi karibuni,tofauti sana na wapinzani wao(Yanga) ambao michezo ya hivi karibuni hawajawa kwenye kiwango cha kuridhisha.
Mtibwa Sugar wanaotumia sana mfumo 4-4-2 na wakati fulani 4-5-1 hasa wanaposhambuliwa sana,ni wazuri katika direct play wakichanganya na long balls na matumizi ya nguvu huku wakienda katika wide formation wanaposhambulia.
Tatizo kubwa kwa Mtibwa linaweza kuwa kwenye idara yao ya ulinzi,  defensive pattens zao sio nzuri sana, makosa binafsi, kushindwa kufanya pre marking imepelekea kuruhusu magoli mengi.
Idara yao kiungo imekuwa ikicheza vizuri,  ni wazi watu kama Haroun Chanongo,Shabani Nditi,Kelvin Friday na Ibrahim Rajab 'Jeba' wanaweza kuwa msaada mkubwa katika mchezo huu.
Idara yao ya ushambuliaji haiko vibaya sana, lakini bado inatakiwa kuongeza umakini kwenye kutumia nafasi.
Kwa upande wa Yanga wanaotumia sana mfumo wa 4-4-2 angle au 4-3-3 vertical wanaweza kuwa na mabadiliko kidogo ya uchezaji hasa kwenye idara yao ya kiungo.
Kukosekana kwa kiungo wa ulinzi wa maana kumeifanya timu kukosa muunganiko mzuri wa kimbinu wakati wa kushambulia. Offensively Yanga imekuwa ikimtegemea sana Thaban Kamusoko kuandaa mashambulizi na kuchezesha timu huku akikosa backup kubwa kutoka kiungo wa chini Technical switch ya Deus Kaseke imeonekana kufeli sana katika michezo ya hivi karibuni,ni wazi mwalim Hans van der Pluijm anaweza akafanya mabadiliko katika idara yake ya kiung.
Idara ya ulinzi ya Yanga bado inaonekana kucheza kwa uelewano mkubwa, japo kidogo hupoteza umakini hasa wanaposhambuliwa sana lakini watu kama Andrew Vicent,Vicent Bossou,Juma Abdul na Haji Mwinyi bado ni wazuri sana kucheza kwenye eneo la ulinzi.
Idara ya ushambuliaji ya Yanga inaonekana kukosa kasi yao ile iliyozoeleka kutokuwa kwenye kiwango bora kwa Donald Ngoma kumeifanya kukosa nguvu kubwa ya kimbinu, ikizingatiwa huyu ndiye Play maker kwenye idara hii, ni wazi hii ni changamoto nyingine kwa mwalimu Pluijm kuelekea katika mchezo huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video