Tuesday, October 18, 2016

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga Africans SC wamewasili salama jijini Mwanza tayari kukabiliana na wenyeji wao Toto Africans katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kesho.

Yanga ambao kwa sasa wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 15 baada ya kucheza michezo 8, wanahitaji ushindi kwa hali na mali ili waweze kujitengenezea mazingira mazuri kuelekea mbio za ubingwa, ambao mpaka sasa mahasimu wao Simba wapo kileleni baada ya kujikusanyia pointi 23.

Wikiendi iliyopita Yanga walikuwa na kibarua kizito mbele ya Azam, mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu.

Wachezaji walioambatana na timu ni Deogratius Munishi, Beno Kakolanya ,Hassan Kessy, Haji Mwinyi,Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Andrew Vicent, Vicent Bossou , Nadir Haroub na Kelvin Yondani.

Wengine ni Saidi Juma , Juma Mahadhi , Saimoni Msuva , Yusufu Mhilu , Mbuyu Twite, Thabani Kamusoko , Deusi Kaseke , Geofrey Mwashuiya na Haruna Niyonzima.

Katika safu ya ushambuliaji ni Obrey Chirwa , Mateo Antony, Amisi Tambwe na Donald Ngoma.

Waliobaki Dar es Salaam ni Juma Abdul aliepata maumivu mechi na Azam , Malimi Busungu matatizo ya kifamilia na Ali Mustafa ambaye bado anauguza jeraha lake.

Timu ipo na bechi lote la ufundi chini ya kocha mkuu Hans Van Pluijm wakijiandaa vyema kushinda mchezo huo kabla ya Jumamosi kuingia mjini Kagera kuvaana na Kagera Sugar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video