Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amejikuta akimpongeza kimakosa nyota wake Mesut Ozil kwa kuchaguliwa kwenye tuzo ya Ballon d'Or ilhali mchezaji huyo hakuchaguliwa.
Wiki hii orodha ya wachezaji 30 watakaowania tuzo hiyo imetolewa, huku Ozil na Alexis Sanchez wakikosekana miongoni mwa wachezaji nane wa Premier League waliochaguliwa.
Orodha ya wachezaji wa Premier League waliochaguliwa ni pamoja na Jamie Vardy na Riyad Mahrez wa Leicester City, Kevin De Bruyne, Sergio Aguero, Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic, Dimitri Payet na Hugo Lloris
"Ni jambo jema sana kwake na kwetu pia, lakini mimi niko kinyume na tuzo hiyo," Wenger alijibu wakati alipoulizwa na mwandishi ambaye pia alikuwa amechanganya juu ya uwepo wa Ozil kwenye tuzo hiyo.
Wenger si muumini mkubwa wa tuzo hiyo, akipendelea zaidi tuzo inayotolewa kitimu kuliko ile ya mchezaji mmoja mmoja.
Wenger aliongeza kuwa hiyo inawafanya wachezaji wengi kupambana kwaajili ya kubeba tuzo hiyo badala ya kutoa msaada wa timu zaidi.
"Hii inafaya wachezaji wengi kuweka akilini zaidi, unaona watu wanajifikiria wao zaidi kwasababu wanapambana ili kushinda Ballon d'Or.
"Soka ni mchezo wa kushirikiana. Tunapaswa kuheshimu jambo hilo ambalo jitihada za timu.
"Nawasisitiza na kuwapongeza wachezaji ambao wanafanya vyema lakini ukiangalia historia kwa undani zaidi, utaona kwamba mara nyingi malengo yamekuwa si kama yale yaliyokusudiwa. Sote tunafahamu fika kwamba wachezaji gani ambao ni bora.
0 comments:
Post a Comment