Saturday, October 15, 2016

Theo Walcott amefunga mabao mawili kati ya matatu na kuipa timu yake ya Arsenal iliyokuwa pungufu mbele ya Swansea chini ya meneja wao mpya Bob Bradley, mchezo uliofanyika Emirates jioni ya leo.

Mshambulizi huyo wa Arsenal na timu ya taifa ya England kwa sasa ametimiza magoli matano kwenye michezo nane, baada ya kufunga magoli mawili leo kwa ustadi mkubwa kufuatia makosa ya Jordi Amat na Jack Cork.

Swansea walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Gylfi Sigurdsson baada ya kiungo wa Arsenal Granit Xhaka kufanya makosa.

Mesut Ozil aliifungia Arsenal bao la tatu baada ya kupata krosi mujarab kutoka kwa Alexis Sanchez, lakini Swansea waliapata goli la pili kupitia kwa Borja Baston aliyeingia kutoka benchi baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Modou Barrow ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa Arsenal leo.

Granit Xhaka alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea faulo mbaya Modou Barrow.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video