Sunday, October 2, 2016

 Na Abdallah Salehe-Mdau wa MPENJA SPORTS-Dar es salaam

Kiujumla mchezo ulikuwa na ushindani kwa kiasi kikubwa japo ulikosa ladha ya ubora kama watu wengi walivyo tarajia. Hii ilitokana na wachezaji kucheza kwa kukamiana na kujikuta wakishindwa kufuata maelekezo ya Walimu wao.
kimbinu na kiufundi, Simba walikuwa bora sana kuliko Yanga, waliweza kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa licha ya kucheza pungufu kwa muda mrefu wa mchezo. Viungo wa Simba Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto na Shiza Kichuya walikuwa na muunganiko mzuri sana na kuweza kuwamiliki wa Yanga kwenye idara ya kiungo.
Tatizo kidogo lilikuwa kwa Kazimoto ambaye muda mwingi alicheza kama kiungo wa mbele na kushindwa kuachia mipira kwa wakati kama winga, Mzamiru alicheza vizuri sana alisaidia kukaba na kusuka vyema mashambulizi.
Kichuya alicheza vizuri kama invisible attacking midfield huyu ndiye alikuwa chanzo cha mashambulizi mengi ya Simba. Kupenda kukaa na mpira kwa viungo kuliifanya timu kushindwa kuwa offensively kwa haraka.
Idara ya ushambuliaji ya Simba haikucheza kwa utulivu na umakini mkubwa, Ibrahimu Ajib alikuwa bora akicheza kama play maker kwenye eneo la ushambuliaji lakini alikosa muunganiko mzuri kati yake na Laudit Mavugo ambaye alicheza kama target man. Kukosa mshambuliaji ambaye ni technical aggressive kuliifanya Simba kushindwa kuwa blast kutokea katikati na kuwanya mabeki wa kati wa yanga kucheza kwa Uhuru.
Idara ya ulinzi ya Simba haikuwa na muunganiko mzuri kiufundi, kushindwa kufanya pre marking na kukosa kasi kulisababisha washambuliaji wa Yanga kutawala sana kwenye eneo la mwisho.
Kwa upande wa Yanga hawakuwa kwenye ubora ule uliozoeleka,walikuwa na makosa mengi kwenye idara ya kiungo, kukosa kiungo mkabaji asilia kuliifanya timu kukosa muunganiko mzuri wa mashambulizi kutokea chini, Mbuyu Twite alicheza deep lying holding midfield na kuacha eneo kubwa kati yake na Kamusoko ambaye alicheza box to box midfield, Deus Kaseke alicheza vizuri kama kiungo kificho wa ukabaji anayetokea pembeni mara nyingi alisaidia blocking na kupokonya mipira.
Idara ya ushambuliaji ya Yanga haikuwa kwenye ubora wake, Donald Ngoma ambaye hucheza kama Auxiliary Attacker ni wazi hakuwa na mchezo mzuri, mara nyingi alishindwa kuiunganisha timu kimashambulizi. Amissi Tambwe alikuwa technical aggressive akishuka kucheza kama false 10 na kuisumbua sana safu ya ulinzi ya Simba.
Idara ya ulinzi ya Yanga ilicheza kwa utulivu na umakini mkubwa hasa mabeki wake wa pembeni waliweza kuzuia mashambulizi mengi ya Simba na kuwa msaada mkubwa kupandisha timu

Subs:
Ni wazi Joseph Omog alikuwa vizuri mara nyingi,  sub zake ziliimarisha timu kimbinu na kiufundi tofauti na Hans van Pluijm ambaye sub yake moja ilikuwa nzuri ya kumtoa kelvin Yondan ambaye alionekana ku panic lakini sub ya Haruna Niyonzima haikuwa na faida kwenye timu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video