Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho
Oktoba 7, 2016 kwa michezo miwili ambako Kagera Sugar itaikaribisha Toto
Africans kwenye Uwanja Kaitaba mkoani Kagera wakati Stand United
itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mbali ya mechi hizo za kesho, Jumamosi Oktoba 8, 2016 pia kutakuwa na
michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya
Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon
itaikaribisha Ndanda FC jijini Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikiialika
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza, kundi A Jumamosi Oktoba 8,
kutakuwa na mchezo kati ya Pamba ya Mwanza na Polisi Dar kwenye Uwanja
wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam es Salaam wakati African Sports
itakuwa mwenyeji wa Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.
Ligi hiyo ya Daraja la Kwanza itaendelea Jumapili Oktoba 9, 2016 kwa
mchezo utakaozikutanisha Ashanti United na Friends Rangers; zote za Dar
es Salaam.
Kadhalika Jumatatu, kutakuwa na mchezo kati ya Mshikamano ya
Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa.
Mchezo huo, pia utafanyika Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.
Kundi B; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya
Kurugenzi ya Iringa na Coastal Union ya Tanga ufakaofanyika huko Mufindi
ukifuatiwa na michezo mitatu siku ya Jumapili Oktoba 9 ambayo Mlale
itacheza na Polisi Moro ya Morogoro huko Uwanja wa Majimaji Njombe Mji
itaikaribisha Kemondo wakati KMC itacheza na Mbeya Warriors kwenye
Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Kundi C; Jumamosi Oktoba 8, mwaka
huu Mvuvumwa ya Kigoma itacheza na Stand United ya Singida wakati Panamo
itapambana na Alliance huku Polisi Dodoma itacheza na Polisi Mara
wakati Jumapili Rhino ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT ya Tanga.
0 comments:
Post a Comment