Tuesday, October 4, 2016

Nyota wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez amesema kwamba, Cristiano Ronaldo ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu.

Ronaldo anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watatu wa mwisho watakaobaki kuwania tuzo hiyo ambayo, mara ya mwisho alishinda mwaka 2014 kufuatia kutwaa Uefa Chamipons League pamoja na Euro 2016 akiwa na Ureno.

Ikumbukwe mwezi uliopita Xavi aliongea shombo juu ya Ronaldo na kumsifu Messi akisema, mtu yeyote ambaye anapenda soka lazima anatambua kuwa Messi ni bora kuliko Ronaldo, kabla ya Ronaldo kumjibu kwa kumwambia Xavi asiongee chochote kwani, hajawahi kushinda hata Ballon d'Or hata moja.

Lakini safari hii Xavi ameamua kumsafishia njia Ronaldo na kusema ni mchezaji mwenye asilimia nyingi zaidi za kushinda tuzo hiyo kwa mara ya nne, japokuwa amemuonya asibweteke kutokana na tuzo hiyo kuwa na ushindani mkali.

"Cristiano Ronaldo ana vigezo vingi vya kushinda tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu, hasa baada ya kutwaa mataji ya Champions League na Euro.

"Lakini pia bila shaka naamini kutakuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwepo wa Messi."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video