Wednesday, October 19, 2016

Pep Guardiola amepinga madai ya moja ya magazeti yaliyodai kwamba, alijaribu kuwasijili Lionel Messi na Neymar wakati wa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

Gazeti la Barcelona Mundo Deportivo kwenye ukurasa wake wa mbele mwezi Septemba liliandika kwamba, Guardiola alijaribu kuwashawishi wachezaji wawili wa Barcelona kujiunga na Man City na mkurugenzi wa City Ferran Soriano alifanya vikao vitatu na kambi ya Messi.

Lakini Guardiola, akiongea kwenye Uwanja wa Nou Camp kuelekea mchezo wa Champions League dhidi ya timu yake ya zamani ya Barcelona, akaamua kutumia muda huo kujibu mapigo juu ya madai hayo.

Amesisitiza hakuwa na mawasiliano na mchezaji yeyote kutoka Barcelona wakati wa usajili wa dirisha la kiangazi, japokuwa amesema kwamba aliongea na mabosi wake hao wa zamani juu ya uwezekano wa kumpata Marc-Andre ter Stegen kabla ya kufanikiwa kumsajili Claudio Bravo

"Sikuwasiliana na mchezaji yeyote kwenye simu," alisema. " Najua kuna vita ambayo imeisha lakini inayooekana kutaka kuanzishwa tena. Sitaki kuelezea kwa undani zaidi dhidi ya kinachozungumzwa. Ingekuwa ni vizuri zaidi endapo stori zote zingetofautishwa. Hakuna mtu yeyote aliyenipigia simu kuuliza kuhusu hili.

"Nilimpigia Thiago wakati ule mwaka 2013 kwasababu mwakilishi wake alikuwa ni kaka yangu na tulifanikiwa kumsajili Bayern. Tuliona fursa ya kufanya hivyo na tuliitumia.

"Miaka kadhaa iliyopita nilimpigia Neymar ili nimsajili Barca. Rais wa wakati huo Sandro Rossell, aliona fursa ya kufanya hivyo na tukampigia simu. Wakati nikiwa New York sikufahamu kama Real Madrid wangeweza pia kumsajili na nikaamua kumpigia baba yake ili kuona kama kulikuwa na fursa hiyo. Niliongea naye na kusema, 'Kama una nafasi ya kufanya hivyo basi ni vyema uende Barcelona' na unaweza kumpigia baba yake Neymar kama unaweza ili kuthibitisha. Na mwisho wa siku aliamua kujiunga na Barcelona.

"Kama mnaongelea kuhusu dirisha hili la usajili, basi hamko sawa, maana sikuwasiliana na Messi,Neymar, Luis Suarez, Busquets wala Iniesta. Sikumpigia yeyote yule. "Kwa upande wa Ter Stegen nilifahamu fika kuwa alitaka kupata fursa ya kucheza muda wote. Tuliwasiliana. Hakuwa na furaha kwa namna alivyokuwa akifanyiwa. Tulihitaji aina ya makipa kama Claudio [Bravo] au Ter Stegen. Kama ningempigia mchezaji mwingine yeyote basi ingekuwa yule ambaye hapati fursa ya kucheza, lakini sikumpigia Leo Messi.

"Kwa kesi ya Messi, ningependa kumwona anaendelea kucheza hapa Barcelona na kustaafia hapa. Kucheza hapa kwa muda mrefu ni jambo jema. Lakini mwenyewe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kama ataamua kubaki hapa au kwenda kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine, kwa mfano pengine angependa watoto wake wazungumze Kiingereza kama ambavyo imetokea kwa sisi wengine. Pengine hali hiyo inaweza kutokea, lakini kama ataamua kuondoka basi lazima kutakuwa na orodha ya vilabu saba au nane hivi ambavyo vitahitaji huduma yake, na hilo litakuwa juu yake kufanya maamuzi. Messi ndiye mwenye maamuzi ya mwisho na si mtu mwingine.

"Nimekuwa na nafasi ya kujielezea mwenyewe. Si kweli kwamba nilimpigia mchezaji yeyote wa FC Barcelona. Naomba mniwie radhi juu ya taarifa hizo.”

Na wakati mwandishi akiajiandaa kuuliza swali jingine, Guardiola aliimkatisha na kuongeza: Oh, na kitu kingine cha kuongezea, Kama hamniamini, kwasababu  nafamu vizuri watu waliondika haya wana uhusiano mzuri na rais Bartomeu, pengine wanaweza kumuuliza. Najua wana namba yake. Pengine anaweza kuwathibitishia ukweli juu ya hii stori.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video