Striker wa Cameroon hajahofia kuweka kitita cha pesa ku-bet akidai timu yake itamaliza katika nafasi 10 za juu.
Samuel Eto’o anayekipiga kwenye klabu ya Antalyaspor timu yake ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ya Uturuki (Turkish Super Lig) kitu kinachosababisha mashabiki kukosa imani ya kusalia kwenye ligi.
Kwenye mchezo wao wa Jumatatu zikiwa zimesalia sekunde tu ili pambano kumalizika na kujihakikishia ushindi wao wa kwanza katika mechi saba, lakini Rizespor ilipata bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Baada ya mchezo Eto’o alikwenda kwa mashabiki waliokuwa wamejaa na hakuahidi tu kwamba timu yao itamaliza ligi ikiwa nafasi ya 10 licha ya mwanzo mmbovu, lakini akaahidi kitita cha euro 100,000.
Shabiki mmoja aliyefahamika kwa jina la Mehmet Akdeniz, alimuuliza Eto’o “Mechi yetu ijayo tunakutana na Besiktas, timu yetu itakuwa kwenye nafasi gani ya kupata ushindi na lini tutapata ushindi wetu wa kwanza?
Eto’o ambaye alijibu kwa kutumia mkalimani akasema: Tutamaliza ligi tukiwa kwenye nafasi 10 za juu za Super Lig, ninasimamia kwa kile nilichokisema pamoja na ahadi yangu.
Samuel Eto'o, 1-1 biten maç sonrası tepki gösteren taraftara: "Bu sezon ligi ilk 10'da tamamlamazsak sana 100 bin euro vereceğim." pic.twitter.com/wIu6tLa49M— Spor Artı ⚽️ (@Spor_Art) October 18, 2016
“Niamini, nitakupa €100,000 endapo tutashindwa kumaliza katika nafasi 10 za juu kwenye ligi.
Eto’o akachukua jina na namba ya shabiki huyo ambaye anasubiri msimu umalizike huku akisubiri pia timu yake ishinde sambamba na kuzitaka €100,000!
0 comments:
Post a Comment