Mario Balotelli amefichua kwamba hakuwa na uhusiano wowote na Jurgen Klopp, ambaye alimwambia mchezaji huyo kuondoka Liverpool kwa mkopo.
Muitaliano huyo alisajiliwa na Brendan Rodgers mwaka 2015 kutoka AC Milan, lakini alishindwa kabisa kuonesha makali yake kabl ya kurudi tena AC Milan kwa mkopo.
Kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Nice, ambapo tayari ameshafunga mabao sita kwenye michezo mitano baada ya kuondoka Liverpool bure kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Na sasa Balotell amefichua kwa kusema kwamba hapakuwa na uwezekano wowote kwake kurudi Anfield kutokana na uhusiano usioridhisha kati yake na Klopp.
"Klopp? Simjui mimi huyo mtu," Balotelli aliiambia Sky Sport Italia. "Aliniambia tu niondoke Liverpool kwa mkopo na baadaye nikarejea kumwambia: 'Asante sana, na kwaheri.'"
0 comments:
Post a Comment