Friday, October 14, 2016

Gerard Pique ameweka wazi kwamba Louis van Gaal alishawahi kuwambia hakuwa vigezo vya kutosha kuichezea FC Barcelona.

Pique ambaye alitokea katika academy ya Barcelona ametoa madai hayo na kuongeza kuwa, bosi wake huyo wa kwanza kabisa katika kikosi cha wakubwa ya Barca alimwambia asingeweza kupata nafasi kikosini hapo.

Akiongea na TV3, Pique amesema: "Huwezi kuelewa kama kocha anakupandisha kwenye kikosi cha wakubwa halafu huyo huyo tena anakudidimiza. Aliniambia kwamba sikuwa na uimara wa kutosha kueweza kucheza timu ya wakubwa ya Barcelona.

"Alinichanganya sana. Kwenye klabu ya Barcelona haturuhusiwi kufanya mazoezi ya Gym mpaka utimize miaka 18. Ilikuwa vigumu sana kwangu."

Tangu wakati huo, Pique amemthibitishia Van Gaal kwamba hakuwa sahihi baada ya kupata mataji lukuki akiwa kama mchezaji tegemeo wa timu hiyo.

Pique (29), ameshacheza michezo zaidi ya 300 katika michuano yote akiwa na Barcelona na kuisaidia kushinda mataji mengi yakiwemo sita ya La Liga na matatu ya Champions League.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video