Star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuzindua hotel yake mpya ni sehemu ya maandalizi ya maisha yake baada ya soka licha ya kusema anajiona bado anauwezo wa kuendelea kucheza kwa miaka kumi ijayo.
Ronaldo alipaa moja kwa moja hadi Lisbon baada ya timu yake kutoka sare ya kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Eibar Jumapili mchana, ambapo baadaye jioni alizindua rasmi hotel inayofahamika kwa jina la Pestana CR7 Lisboa hotel.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Ronaldo alimshauri rais wa Real Madrd Florentino Perez kuwa anatakiwa amuongeze mkataba wake ili andelee kucheza hadi atakapofikisha miaka 40.
“Maisha si mpira kwenye soka pekee,” alisema Ronaldo. “Licha kwamba mpira ndio kitu nachokipenda, lakini natakiwa nifikirie kuhusu maisha yangu ya baadaye. Sina muda mwingi, ni kama miaka 10 au chini ya hapo, kwahiyo ni lazima niangalie mbele.”
Hotel hiyo yenye vyumba 82 ni ya pili kufunguliwa chini ya ushirikiano wa Ronaldo na mfanya biashara mkubwa wa Ureno Pestana, yakwanza ikiwa Madeira kwenye kisiwa ambacho ndipo Ronaldo alipozaliwa na kukulia.
Bei ya vyumba katika hotel ya Pestana CR7 Lisboa ni kuanzia €200 kwa usiku mmoja hadi €1,250 kwa vyumba vya ghorofa ya juu kabisa ambavyo vina HD TV ya inchi 48, PlayStation 4 na vitu vingine kibao.
Website ya Pestana CR7 Lisboa inaelezea namna ambavyo wageni wanaweza kupata huduma na kufurahia maisha kwenye hotel hiyo.
Inaripotiwa kiasi cha €15 million zimetengwa kwa ushirikiano wa Pestana na Ronaldo kwa ajili ya kuongeza hotel nyingine mbili moja katika jiji la Madrid na nyingine New York.
Nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kumiliki hotel yangu,” anasema mchezaji huyo wa zamani wa Sporting Lisbon wakati wa uzinduzi huo. “Sasa ninazo mbili, najisikia faraja ipo Lisbon jiji ambalo ni sehemu ya historia ya maisha yangu, nilishawahi kucheza hapa.
0 comments:
Post a Comment