Sunday, October 9, 2016

 

Na Ally Kamwe
SHIZA Ramadhani Kichuya, wanadamu tunaishi mara moja tu. Hakuna mwenye ahadi ya kufika kesho kama ambavyo hakuna mwenye uwezo wa kurudi jana.
Ukipata nafasi ya kuishi, usifanye makosa, Ishi kweli.
Wakati una mapito yake, kama isivyodumu Mbalamwezi ya mwandamo ndivyo kitakavyopotea kila ambacho kinaonekana bora kwa wakati husika. Yuko wapi Mike Tyson?
Yuko wapi DMX? Yuko wapi Paul Gascoigne ‘Gazza’? Wote wamemezwa na wakati. Hakuna shujaa wa kudumu duniani, Ishi kweli Shiza Kichuya.
Inaaminika mwanadamu anapofika mwisho, hukumbuka zaidi mambo asiyoyafanya kuliko aliyofanya. Sikiliza tu stori za Mr Nice na Dudubaya wakati huu na utajifunza kitu, thamani ya wakati ipo kwa aliyeuthamini, Ishi maisha yako yote sasa Kichuya.
Hakuna nafasi nyingine tena zaidi ya hii, huu ni wakati wako na ni mwaka wako wa kung’ara na kuzibeba ndoto zako ulizowahi kumuahidi Kanali Iddy Kipingu pale Lord Baden.
Maisha ya Bongo yanakimbia kasi mno kuliko maisha ya sehemu yoyote ile duniani, kimbizana nayo. Usichoke wala usithubutu kusimama kwa zawadi za gari na ofa za mafuta sheli.
Ulichokifanya dhidi ya Yanga ni kikubwa zaidi ya pointi moja uliyoipeleka Msimbazi, najua umefurahisha wengi na nafsi yako imefarijika. Nilipenda pia ulivyopokelewa kule Morogoro.
Vyote hivyo ni ishara kuwa upo mwanzoni mwa safari, visikufanye ukashusha mabegi na kuamini umeshafika, bado sana Kichuya.
Bahati nzuri upo sehemu salama kwa sasa, iwe tunaamini au hatuamini lakini ukweli ni kuwa Simba ni sehemu sahihi zaidi kwa wasafiri wa Ngambo ya mbali, waliosafiri na kufanikiwa walitoka kwenye bandari ile.
Watumie Simba kufika kama ambavyo wao wamepanga kukutumia uwafikishe safari yao. Kuwafunga Yanga, Ruvu Shooting hakutatosha kuonekana na walio kando ya bahari, unahitaji jitihada zaidi.
Pambana sasa Simba wapate mafanikio zaidi, wafikishe kwenye michuano mikubwa kisha usimame na uuze jina lako.
Naamini ubora wa mabao yako sita ulioyafunga VPL, ungetosha kukuuza mbali kama ungeyafunga matatu tu kwenye michuano ya CAF. Wapeleke Simba safari yao, uanze safari yako.
Kwa sasa Taifa linasimama nyuma yake, ni mwendawazimu pekee atakayepewa ‘Taifa Stars’ na akashindwa kumjumuisha Kichuya kwenye orodha ya wachezaji 11 watakaoanza mchezo wowote ule, uwezo wake unajieleza vyema!
Sina mengi kwa leo, lengo langu ni kutaka kukumbusha tu kuwa, Jua la Magharibi lipo kwa ajili ya kuizima nuru ya dunia. Ally Kamwe hapa nakusalimia kijana mwenzangu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video