Wednesday, October 26, 2016

Nyota ya mshambuliaji wa Yanga Mzambia Obrey Chirwa imeendelea kung'ara baada ya kufunga goli muhimu katika mchezo wa kiporo Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Wakicheza kwa mara ya kwanza chini ya Juma Mwambusi ambaye anakaimu nafasi ya kocha mkuu baada ya Hans van der Pluijm kujiuzulu, Yanga walionekana kuwa na hamu ya goli mapema tu baada ya mwamuzi kupuliza filimbi na kushambulia mara kwa mara goli la JKT Ruvu huku kipa wao Yusuf Kipao akifanya kaziya ziada ya kuokoa hatari hizo.

Mapema tu dakika ya 6 Obrey Chirwa aliiandika Yanga bao la kwanza baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Simon Msuva kufuatia makosa yaliyofanywa na beki wa JKT Ruvu Salim Aziz Gilla ambaye aliteleleza katika harakati za kuokoa mpira.

Katika nyakati tofauti, wachezaji wa Yanga Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Simon Msuva na Hassan Kessy walikaribia kuifungia timu yao magoli lakini juhudi zao hazikuzaa matunda.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa kifua mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kucheza kwa kuviziana, JKT Ruvu waitafuta goli la kusawazisha huku Yanga wakisaka bao la pili.

Dakika ya 58 Donald Ngoma alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Amissi Jocelyn Tambwe.

Dakika chache tu akiwa uwanjani,Tambwe aliipatia Yanga bao la pili baada ya kuwachomoka mabeki wa JKT Ruvu na kumchambua kwa uzuri kipa Kipao.

Dakika ya 67 JKT Ruvu walipata bao lakini mwamuzi alikataa baada ya mfungaji Nurdin Mohamed kufunga kwa mkono.

Simon Msuva aliipa Yanga bao la tatu dakika ya 83 kufuatia pasi nzuri ya kuchop kutoka kwa Amissi Tambwe.

Baada ya bao hilo, Msuva alifanyiwa mabadiliko na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi.

Amissi Tambwe kwa mara nyingine alifunga bao lake la pili kwenye mchezo na la nne kwa Yanga dakika ya 90 baada ya uzembe wa beki wa JKT Ruvu na kuhitimisha karamu ya mabao kwenye mchezo huo.


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video