Friday, October 14, 2016

BAADA ya Saimon Msuva kufunga bao katika ushindi wa 3-1 waliopata Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar Jumatano ya Juma hili Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, zilitoka Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Yanga wakiwemo Viongozi kuwa Mshambuliaji huyo amefikisha mabao 50 ndani ya Klabu hiyo katika mashindano yote.
Hata hivyo aliyewahi kuwa Mwalimu wake na katibu mkuu wa Yanga pia, Dkt. Jonas Tiboroha ameibuka na kusema Takwimu hizo haziko sawasawa.
Kwa mujibu wa takwimu zake yeye,  Dk. Jonas Tiboroha, aliyemuibua Simon Msuva kwenye kituo chake cha WAKATI UJAO, anasema: "Simon Msuva ana mabao 53. 
Cha ajabu Yanga wao wamesema Msuva alianza kucheza Yanga 2013/14 na bao lake la kwanza alifunga dhidi ya URA kwenye Kagame. Jiulize, ni Kagame gani ambayo Yanga wamecheza kuanzia 2013/14? Utakuta ni ile ya 2015 ambayo Azam walikuwa mabingwa. Ina maana hapo kabla Msuva hakuwahi kufunga? Kumbukumbu zangu, Msuva kajiunga na Yanga msimu wa 2012/13 na bao lake la kwanza alifunga dhidi ya JKT Ruvu Sept. 22, 2012. Siku hiyo Yanga walishinda 4-1".
MPENJA SPORTS inafuatilia habari hii ili kutoa mkanganyiko huu....

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video