Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon ambaye pia alikuwa nahodha, Rigobert Song amepatwa na maradhi ya kupooza na amekimbizwa hospitali huko mjini Yaounde, Kameruni.
Song ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Liverpool na West Ham United amepatwa na hili ikiwa ni ghafla sana. Ikumbukwe pia kuwa huyu ni mjomba wa mchezaji wa zamani wa Arsenal, Barcelona na West Ham United, Alexander Song.
Rigobert Song ambaye pia mpaka anapatwa na maradhi haya alikuwa kocha wa timu ya Taifa ya wakubwa ya Chad, amekumbwa na ugonjwa wa kupooza ambao kitaalamu unafahamika kama cerebral aneurysm, huku pia akisemekana kuwa mahututi sana.
Ulimwengu wa soka upo katika maombi kumwombea mwanasoka huyu wa zamani huku wachezaji kama Patrick Mbona, Samuel Etoo, Jamie Carragher, Stan Collymore pamoja na Robbie Fowler ambao Waliwahi kucheza naye katika ngazi tofauti za vilabu mpaka Timu ya Taifa wakiwa ni watu wa awali kuwahi kutuma salamu za pole na kumwombea kupitia mitandao yao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment