Klabu ya Yanga SC imetuma maombi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kutumia Uwanja wa Amaan kwaajili ya michezo yao mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Taarifa rasmi kutoka kwa Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit imesema kwamba, hatua hiyo inafuatia Serikali kuizuia klabu hiyo pamoja na mahasimu wao, Simba SC kutumia Uwanja wa Taifa.
Yanga imeiandikia barua Wizara ya Habari Utakii na Michezo Zanzibar kuomba kuhamia Uwanja wa Amaan, baada ya kufungiwa kwa Uwanja wa Taifa.
Tayari Wizara hiyo imethibitisha kupokea maombi hayo na imeahidi kuyafanyia kazi
0 comments:
Post a Comment