Thursday, October 13, 2016


Mshambuliaji wa Stand United, Mnigeria, Chidiebere Abasirim,  inaendelea vizuri na matibabu baada ya kupata majeraha mabaya katika mechi ya jana ya ligi kuu soka Tanzania Bara ambayo timu yake ya Stand United ilishinda bao moja kwa bila dhidi ya Azam FC Uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Chidiebere, aliruka kuwania mpira wa juu na mlinzi wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris ambapo Aggrey Morris alimgonga kwa kiwiko kabla ya kuanguka vibaya .


Nyota huyo alitibiwa Uwanjani kwa dakika nyingi, lakini jitihada ziligonga mwamba na jopo la madaktari wa Stand United wakishirikiana na wa Azam FC walilazimika kumuondoa Uwanjani kumpeleka Hospitali kubwa kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, habari zilizotufikia ni kuwa Wachezaji wa Azam FC, wakiongozwa na kocha mkuu, Seven Hernandez wamemtembelea Chidiebere.
Miongoni mwao wanasoka hao ni Aggrey Morris aliyehusika kwenye tukio, nahodha John Bocco,  Bruce Kangwa na David Mwantika.

Naye Kamishina wa mchezo huo,  Alfred Lwiza, (Pichani kushoto)  amemjulia hali  Chidiebere aliyelazwa katika Hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga .
Chidiebere anaendelea na matatibabu ambapo baada ya kufikishwa hospitalini hapo alishona sehemu aliyochanika vibaya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video