Na Abdallah Salehe, Mdau wa MPENJA SPORTS
MECHI nyingine kali ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara leo ni kati ya Stand United na Azam FC itakayochezwa kuanzia saa 10:30 Jioni Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Nadhani huu utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa na
hautakuwa rahisi kwa pande zote kwa kuzingatia ubora wa vikosi na
mabenchi ya ufundi ya pande zote. Pia nafasi katika msimamo wa ligi ni
changamoto kubwa kuelekea katika mchezo huo.
Azam inayonolewa na kocha Mhispania, Zeben Hernandez, ni wazi itaingia
uwanjani kuziwinda Pointi tatu muhimu ili kuweza kusogea nafasi
za juu kwenye msimamo wa ligi, wakati Stand wao watahitaji ushindi ili kujiimarisha zaidi kwenye nafasi ya pili au kupanda kileleni kutegemeana na matokeo ya Mbeya City na Simba leo.
Stand kwasasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 8, huku Simba wakiongoza Ligi kwa alama 17 walizovuna kwenye michezo 7.
Azam inayotumia mfumo wa 4-4-2 na 4-5-1 wanaonekana
kuimarika kiuchezaji, wakicheza soka la kueleweka kuanzia mwanzo mpaka eneo la hatari la timu pinzani.
Idara ya kiungo ya Azam itatakiwa kubadilika kidogo aina
yao ya uchezaji kwa kupunguza square passes ambazo kimbinu hazina
madhara sana kwa mpinzani. Offensively Pattens watatakiwa kufanya kwa
haraka sana ili kufika mapema kwenye attacking zone ya Stand United.
Nafikiri mtu kama Ramadhan Singano anaweza kuwa msaada mkubwa
kwenye eneo hili akicheza kama creative midfielder, huyu anaweza kutoa
option nyingi kwenye idara kiungo. Ni wazi Himid Mao atakuwa kiongozi eneo hili akicheza kama defensive midfield ikizingatiwa huyu ni
ball winning midfield mzuri sana.
Sulum Abubakary ataendelea kuwepo kama
central midfield akitakiwa kuichezesha timu. Licha ya uimara wa Azam kwenye safu ya kiungo, bado watatakiwa kuongeza umakini ili kuwadhibiti viungo wa Stand United.
Idara ya ushambuliaji ya Azam inaonekana kukosa umakini wa
kutumia nafasi za kufunga na kucheza sana nje ya box la mpinzani na imekuwa
tatizo linaloisumbua sana safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Hivyo katika
mchezo huu watatakiwa kubadilika sana ili kuweza kuipenya ngome ya Stand. Give and go passes zinaweza kuwa na faida kwa.
Idara ya ulinzi ya Azam imeonekana kukosa muunganiko mzuri
wa kimbinu, kushindwa kufanya marking kwa wakati imepelekea kuruhusu
magoli mengi, hivyo watatakiwa kuongeza umakini ili kuwadhibiti
washambuliaji wa Stand United ambao mara nyingi hucheza ndani ya box na
kulazimisha makosa.
Kwa upande wa Stand United inayonolewa na kocha, Mfaransa, Patrick Liewig ,ni wazi wataingia katika mchezo huu kuhakikisha wanapata alama
ili waendelee kusalia kujikita nafasi za juu kwenye msimamo wa lig.
Stand United inayotumia sana mfumo wa 4-4-2 wakicheza
katika narrow formation ni wazuri sana kwenye half way offensive ambapo hukataa kujilinda muda wote.
Ni wazi ubora wa Stand unaanzia kwenye idara
yake ya ulinzi, watu kama Aron Lulambo, Adeyum Ahmed, Revocatus Richard na Ibrahim Isaac, wamekuwa na muunganiko mzuri kwenye idara ya ulinzi.
Idara ya kiungo ya Stand United ni sehemu ambayo viungo wa Azam
watatakiwa kuwa makini sana ikizingatiwa Stand ni wazuri sana kwenye cut
off, hivyo watalazimisha kuua key players wote wa Azam. Jacob Masawe na Amri Kiemba ni wazuri sana kwa kuchezesha timu na kupiga long balls au
deep Penetration passes hivyo ni watu wanaotakiwa kuchungwa sana.
Idara ya ushambuliaji ya Stand ni wazuri sana kwenye
matumizi ya counter attack na mara nyingi hupenda kucheza ndani ya box
ili kumlazimisha mpinzani afanye makosa, hivyo walinzi wa Azam watatakiwa
kuwa makini sana na aina hii ya mbin.
NB:
Stand United ni timu inayocheza kwa nidhamu kubwa huku fighting spirit yao ikiwa nzuri sana. Ni wazi Azam watatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kupata matokeo bora huku ubora wa sehemu ya kuchezea'pitch' ikiwa changamoto kubwa kwao.
Stand United ni timu inayocheza kwa nidhamu kubwa huku fighting spirit yao ikiwa nzuri sana. Ni wazi Azam watatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kupata matokeo bora huku ubora wa sehemu ya kuchezea'pitch' ikiwa changamoto kubwa kwao.
0 comments:
Post a Comment