Na Hissan Salum
Morali yetu imeshuka , wengi tukiamini timu yetu imepoteza mwelekeo! Zile amsha amsha hazipo tena , redioni wanaosikika ni wale wanaoisema mabaya Yanga SC hata magazetini habari zetu sio zile zenye malengo chanya . . Mzee Akilimali, Mkemi wanapewa muda mwingi maredioni ili kutuvuruga! Baadhi ya waandishi magazetini wamepewa kazi maalum kuandika habari zisizo, miongoni mwao
ni wale waliopo katika orodha ya saidia Simba ishinde, tambueni kuwa hao wamelipwa, wamelipwa kutuvuruga, wamelipwa kuhakikisha ufalme wetu katika ligi ya Tanzania unatoweka wengine wanafanya kwa kuwa mazuri yetu yanawaumiza . . Hatupaswi kuwa wanyonge, hatupaswi kukubali hali hii.
Huu ni muda wa kudhihirisha maana halisi ya Mwananchi, na sifa kubwa ya shabiki, mpenzi na mwanachama wa Yanga ni kuwa hutanguliza maslahi ya klabu yake mbele, daima huipigania klabu yake! Tusiwe watu wa kuungana kufurahi pamoja wakati wa ubingwa huu ni muda muafaka wa kudhihirisha kuwa hata tupitiapo magumu bado tutawaunga mkono wachezaji wetu, waalimu wetu, viongozi wetu na wale wote wanaoitakia mema klabu yetu.
Kaka yangu Jerry Murro alipenda kunukuu msemo huu kuwa 'NGARIBA HAOGOPI MKOJO' akimaanisha kuwa changamoto ndogo haziwezi kumtisha bali atazikabili na kuzimaliza, sasa Wananchi hatupaswi kukimbia kivuli chetu wala kukinyooshea kidole kwa mabaya , Yanga ni sisi na sisi ndio Yanga_____ Oktoba 23 (Jumapili) tutakuwa na mkutano mkuu wa dharula - Jangwani, twendeni tukaongelee pale mambo yetu.
Itakuwa aibu kubwa kushindwa kutetea ubingwa wetu, aibu zaidi kupoteza ubingwa mbele ya watani zetu . . Tuna kikosi ambacho kinastahili kuwa mabingwa kwa msimu wa tatu mfululizo, tuna uongozi na waalimu bora zaidi kufananisha na vilabu vingine pia tupo mashabiki wengi Tanzania nzima tunaoweza kuishangilia klabu yetu uwanja wowote ule katika mkoa wowote ule ili kuhakikisha tunakuwa mchezaji wa 12 hodari. Kumbuka "If you don't fight for what you want, don't cry for what you lost."
Tushawajua adui zetu hatupaswi kuumizwa na fitna zao , wahenga walisema ukimjua adui yako ni mwanzo mzuri wa kushinda vita.
Nakutakia asubuhi njema na mchezo mwema dhidi ya Toto Africans jioni ya leo.
Follow Instagram : hissansalum
0 comments:
Post a Comment