Saturday, October 29, 2016

Simba imepata ushindi wake wa kwanza mbele ya Mwadui FC tangu timu hiyo inayomilikiwa na mgodi wa almasi ilivyopanda kucheza ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2015-2016. Simba imeifunga Mwadui magoli 3-0 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na kutoka na pointi tatu kwa mara ya kwanza dhidi ya Mwadui.

Kabla ya mchezo wa leo, Simba na ilishindwa kupata ushindi katika mechi mbili za msimu uliopita huku ikichezea kichapo cha goli 1-0 kwenye uwanja wa taifa wakati wa mchezo wa marudiano. Mchezo wa kwanza uliozikutanisha klabu hizo ulipigwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga na Simba kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1.

Mtibwa yang’ara ndani ya Simba

Ibrahim Mohamed amefanikiwa kufunga kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa kujiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar. Ibrahim amefunga magoli mawili na kusaidia goli moja lililofungwa na Shiza Kichuya.

Hadi sasa, wachezaji wote waliosajiliwa na Simba msimu huu wakitokea Mtibwa Sugar (Mzamiru Yassin, Ibrahim Mohamed na Shiza Kichuya) ila mmoja ameshaifungia timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi.

Watatu hao wameshafunga magoli 14 kwa pamoja tangu walipoanza kuichezea Simba (Shiza Kichuya (8), Muzamiru Yassin (4) na Ibrahim Mohamed (2) na kuisaidia Simba katika magoli 24 iliyofanikiwa kufunga katika michezo 12 hadi sasa.

Kichuya abari ya mujini

Kichuya bado ameendelea kupasia kamba katika mfululizo wa mechi za ligi kuu Tanzania bara, tayari ameshapasia nyavuni magoli 8 magoli mawili mbele ya Amis Tambwe wa Yanga mwenye magoli 6 katika orodha ya wafungaji wa VPL hadi sasa. Kichuya pia anaongoza kwa kutupia nyavuni ndani ya klabu yake.

Mohamed Ibrahim aondoa gundu

Alikuwa amebaki peke yake kufunga kati ya wachezaji waliosajiliwa kutoka Mtibwa Sugar. Hatimaye amefunga kwa mara ya kwanza magoli mawili kwenye ushindi wa kwanza wa klabu yake dhidi ya Mwadui FC. Alianza kucheza akitokea benchi lakini amefanikiwa kumshawishi kocha wake Joseph Omog na tayari ameshaanza kwenye mechi kadhaa za klabu yake.

Huyo mavugo vipi?

Alitolea katikati ya kipindi cha kwanza na nafasi yake ikachukuliwa na Ame Ali. Mavugo ni moja wachezaji walitarajiwa kufanya makubwa ndani ya Msimbazi kutokana na usajili wake ulivyokuwa. Huenda babo anahitaji kupewa muda zaidi ili kuendana na mbinu na mfumo wa kocha Joseph Omog ambaye mara kadhaa amemuanzisha benchi na Blagnon kuanza kwenye kikodi cha kwanza.

Dondoo

Simba inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 12 hadi sasa huku ikiendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo, imeshinda mechi 10 na kutoka sare mara mbili.

Simba imeshinda mechi zake zote (5) za mwisho bila kuruhusu kufungwa goli hata moja (5 clean sheets) huku ikiwa klabu iliyofungwa magoli machache hadi sasa (magoli matatu).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video