Klabu ya Simba imemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kutokana na uharibifu wa uwanja wa
taifa uliofanywa na mashabiki wa Simba wakati wa mchezo wa ligi kuu
Tanzania bara dhidi ya Yanga.
Ofisa habari wa Simba Haji Manara amesema, wanaomba radhi kwa Mh.
Magufuli kwasababu ndiye anayesimamia mali zote za nchi hii kwa niaba ya
wananchi wote.
“Rais wa klabu ya Simba, Kamati ya Utendaji Secretariat, benchi la
ufundi na wachezaji, wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba wanaomba
radhi kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh. Nape Nnauye
kwa kitendo kisicho cha kiungwana kilichofanywa na baadhi ya mashabiki
wetu kwenye mchezo wa October Mosi dhidi ya Yanga.”
“Tumeona kuna umuhimu sio kumuomba radhi Mh. Waziri Nauye na TFF
lakini tumeona tumuombe radhi na Rais wetu. Hizi ni rasilimali zetu
zinazojengwa kwa kodi zetu, Serikali inatumia gharama kubwa kuziendesha
rasilimali hizi. Ni upuuzi wa kiwango cha juu kufanya kitendo kama
kile.”
“Nilishatoa taarifaya kuomba radhi mara tu baada ya mchezo ule na
Rais wa klabu alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akiomba radhi.
Tunamuomba radhi Rais wa nchi kwasababu yeye anasimamia mali za nchi
hii kwa niaba ya wanachi wote.”
0 comments:
Post a Comment