Na Abdallah Salehe-Mdau wa MPENJA SPORTS
Natarajia mchezo utakuwa na ushindani mkubwa kwa kuzingatia
ubora wa vikosi vya timu zote na nafasi katika msimamo wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Simba inayoongoza msimamo Ligi
ikijikusanyia alama 20 baada ya kucheza michezo 8 ni wazi itaingia
katika mchezo huo kusaka alama 3 muhimu ili kuendelea kujiimarisha
zaidi kileleni.
Simba inayonolewa na kocha Joseph Omog, Raia wa Cameroon
inaonekana kuimarika vyema kimbinu na kiufundi.
Wakitumia mfumo wa 4-4-2 au
4-3-3 ni wazuri sana kwa kumiliki mpira huku wakifanya pressing game
ili kumnyima mpinzani eneo kubwa la kushambuli.
Ubora wa Simba upo kwenye idara yake ya kiungo huku mzizi wa
timu uko kwa watu kama Jonas Mkude,Mzamiru Yassin na Mwinyi Kazimoto.
Nyota hawa wamekuwa na
muunganiko mzuri wa kimbinu katika kusukuma mashambulizi na kuua
mipango ya timu pinzani. Ni wazi Kagera Sugar watatakiwa kuwa makini sana
na aina ya uchezaji ya viungo wa Simba.
Idara ya ushambuliaji ya simba bado inaonekana kucheza kwa
utulivu mkubwa,kutokana na uimara wa kimbinu kutoka kwa viungo wao wa
nyuma,muunganiko huu huwafanya washambuliaji wa Simba kuwa hatari sana
kwenye eneo la mwisho, watu kama Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib wamekuwa
wakifanya kazi kubwa ya kutengeneza nafasi. Fredrick Bragnon huyu ni
technical aggressive, anajua jinsi gani ya kucheza kama mshambuliaji wa
kati, ni wazi walinzi wa Kagera Sugar watahitaji msaada mkubwa kutoka kwa
viungo wao ili kuua muunganiko huu wa kimbinu.
Idara ya ulinzi ya simba imekuwa na muunganiko mzuri licha
ya kukosa kasi kwa watu kama Method Mwanjali,Nolvaty Lufunga na Janvier Besala Bokungu, lakini uzoefu umekuwa ukiwasaidia sana kupunguza idadi ya makosa
huku tatizo lao kubwa likiwa ni kushindwa kucheza mipira juu.
Kagera Sugar inayoshika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi
hiyo ikijikusanyia alama 15 katika michezo 9 iliyocheza ni wazi itaingia
katika mchezo huo kusaka alama 3 muhimu ili kujiweka mazingira
mazuri zaidi.
Kagera Sugar inayonolewa na kocha Mecky Mexime mara nyingi
hutumia mfumo wa 4-4-2 Diamond, nayo sio timu ya kubeza, ni wazuri sana
kwenye kumiliki mpira na kujenga mashambulizi ya kasi kutokea pembeni
ikizingatia kwasasa wanaonekana kuimarika kwenye pattens zao uchezaji.
Idara ya kiungo ya Kagera Sugar imekuwa na makosa ya
kiufundi hasa kwenye marking, mara nyingi huruhusu timu
kushambuliwa, kushindwa kufanya pressing na kupoteza mipira kutokea
katikati ya uwanja. Hii ni aina ya makosa ambayo yamekuwa yakiigharimu
timu, ni wazi katika mchezo huo watatakiwa kuwa makini sana na aina ya
uchezaji wa viungo wa Simba.
Idara ya ushambuliaji ya Kagera Sugar bado inaonekana kukosa
muunganiko mzuri wa kimbinu kutoka kwa viungo wao, umakini kwenye kutumia
nafasi ni tatizo linalo isumbua sana timu hii. Ni wazi katika mchezo huo
watatakiwa kuongeza umakini ili kuweza kutumia vema nafasi
zitazopatikana, matumizi ya high ball yanaweza kuwa na faida kubwa kwao
kwa kuzingatia walinzi wengi hawana kasi nzuri kwenye marking.
Idara ya ulinzi ya Kagera bado kiufundi haiko vizuri sana, hushindwa kujipanga kwa wakati kufanya pre marking ni aina ya makosa
ambayo yamesababisha kuruhusu magoli mengi.
Mwalimu Mecky Mexime
atatakiwa kujipanga vyema safu hii ili kuweza kuwakabili washambuliaji wa Simba.
Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib ni wachezaji wa kuchungwa sana
kwenye mchezo huo, umakini kwenye mipira ya kutengwa unahitajika sana kwa
maana Simba wanaonekana ni wazuri kwa matumizi ya aina hii ya mipira.
0 comments:
Post a Comment