
Bao linalozungumziwa hapo ni lile la dakika ya 69 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Msuva mwenyewe pia kupitia akaunti yake ya Instagram, alitoa taarifa ya shukrani kwa wote walimsaidia kufikia mafanikio hayo.
Taarifa hizi zilimshtua katibu mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga, dk. Jonas Tiboroha.
Kwa mujibu wa takwimu za Dk. Tiboroha, aliyemuibua Simon
Msuva kwenye kituo chake cha WAKATI UJAO, mchezaji huyo ana mabao 53 na
Yanga.
Dk. Tiboroha anasema yeye amekuwa akimfuatilia Msuva kwa
sababu ni mchezaji wake aliyemlea tangu mdogo kabla hajajiunga na
akademi ya Azam FC.
Kinachotia shaka zaidi ni maelezo ya Yanga kuhusu Msuva
kwenye pongezi zile, klabu hiyo imesema Msuva alijiunga na Yanga 2013/14
na bao lake kwanza alilifunga dhidi ya URA ya Uganda kwenye Kagame Cup!
Swali la kujiuliza, ni Kagame gani ambayo Yanga wamecheza kuanzia 2013/14?
2013 Kagame ilifanyika Sudan na Yanga kama mabingwa
watetezi hawakwenda kutetea ubingwa wao kutokana na zuio la serikali juu
ya usalama.
Kagame ya 2014 ilifanyika Rwanda na Yanga hawakwenda kwa
sababu ya kujichanganya juu ya kikosi cha kukitumia kwenye mashindano
hayo.
Kagame ambayo Yanga ilishiriki ni ile ya 2015 ambayo Azam walikuwa mabingwa. Ina maana hapo kabla Msuva hakuwahi kufunga?
Kwa kuwasaidia Yanga, Msuva alianza kuitumikia klabu hiyo
2012/13 na bao lake la kwanza alifunga dhidi ya JKT Ruvu Sept 22, 2012.
Yanga walishinda 4-1.
0 comments:
Post a Comment