Sunday, October 2, 2016

 TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeshindwa kukata tiketi ya Fainali za Afrika mwakani Madagascar baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji Kongo - Brazzaville leo Jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Debat mjini Brazaville katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo.  
Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inatolewa kwa bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3, kufuatia kushinda 3-2 katika mechi ya kwanza wiki mbili zilizopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 "Mtuwie radhi, hata sisi mwanzo tuliambiwa matokeo ni bila bila, hata mitandao yote kweli ilionyesha bilabila. Lakini mwisho tumepewa taarifa ambazo ni za uhakika kwamba tumefungwa kwa bao moja, dakika nne za nyongeza," alisema Celestine Mwesigwa, katibu mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF.
 Hii inakuwa mara ya pili Serengeti Boys kuikosa kosa tiketi ya fainali za Afrika baada ya mwaka 2005 kufuzu fainali za Gambia, kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabawe, lakini ikaenguliwa kwa kashfa ya kumtumia mchezaji aliyezidi umri, Nurdin Bakari aliyekuwa anachezea Simba SC wakati huo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video