Mfululizo wa ushindi katika mechi sita za Premier League kwa upande wa Arsenal umeishia leo baada ya kulazimishwa suluhu na Middlesbrough katika Uwanja wa Emirates, lakini hata hivyo alama moja waliyopata imetosha kuwapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger leo alikuwa akisherehekea miaka 67 ya kuazaliwa na kushuhudia timu yake ikitawala mchezo lakini ikishindwa kuibuka na ushindi.
Arsenal walifanya majaribio matano yaliyolenga lango la wapinzani wao, lakini kipa Victor Valdes alikuwa makini kuokoa michomo hiyo hasa kutoka kwa Alexis Sanchez.
Kipa wa Arsenal Petr Cech alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo miwili ya kichwa kutoka kwa Gaston Ramirez pamoja na Adama Traore bila kusahau Alvaro Negredo.
Arsenal walipata goli dakika za mwisho kupitia kwa Mesut Ozil, lakini mwamuzi alikataa na kudai Ozil aliotea kabla ya kufunga.
0 comments:
Post a Comment