Sakata la mabadiliko ya benchi la ufundi Yanga hasa baada ya kujiuzululu kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Mholanzi Hans van der Pluijm limegusa hadi maafisa wakubwa wa serikali.
Jana usiku wakati Yanga wakiwa kwenye mapumziko kuelekea mchezo wao leo dhidi ya JKT Ruvu, Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo Mwigulu Nchemba alikutana na wachezaji na kuwapa nasaha mbalimbali juu ya mustakabali wa klabu kutokana na mambo yanayotokea wakati huu.
Nchemba aliwaambia wachezaji wanatakiwa wahakikishe wanashinda michezo yote bila kujali nini kimetokea wakati huu, kwani matatizohuwa yanapita lakini ukipoteza mchezo fursa huwa haijirudii.
" Nimepita kuwaona vijana kambini kuwaweka sawa wajue tukipoteza point hazirudi. Matatizo yatapita ila kama tumeshapoteza point hata matatizo yakiisha pointi hazirudi." alisema Nchemba.
0 comments:
Post a Comment