Andre Villas-Boas amefichua mbivu na mbichi juu ya mahusiano yake na bosi wake wa zamani wa Jose Mourinho punde tu baada ya kuachana naye na kuamua kujitegemea mwenyewe.
Baada ya wote kwa pamoja kuanza shule ya soka chini ya marehemu Sir Bobby Robson, ilikuwa ni suala gumu kuwatenganisha wawili hao, ambapo Villas-Boas alikuwa mtu muhimu kwenye timu ya uchambuzi ya Mourinho (analytical backroom staff) wakati akiwa Porto, kabla ya kumfuata Chelsea na baadaye Inter Milan.
Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyodizi kuchota ujuzi kwa bosi wake huyo na hamu ya kusimama mwenyewe ikazidi kuongezeka. Baada ya muda aliamua kuachana na Mourinho wakati huo akiwa Inter Milan na kwenda kuanza maisha mapya katika klabu ya Academica baada ya kushindwa kupata nafasi kunako klabu ya Braga.
Na katika wakati huo ndipo uhusiano wake na Mourinho ulipoanza kuwa mashakani, Mourinho akihisi msaidizi wake huyo wa zamani angeweza kumpa changamoto kubwa katika tasnia hiyo. Mambo yalizidi kunoga zaidi pale ambapo alipata fursa ya kuzifundisha timu mbili za Porto na baadaye Chelsea, timu ambazo Mourinho aliwahi kuzifundisha.
Licha ya uhusiano wao kuingia walakini baada ya kuanza maisha yake nje ya Mourinho, Villas-Boas bado anakumbuka hali tete aliyokumbana nayo mwanzoni kabisa wakati anaanza kufanya kazi na Mourinho, japokuwa mambo yalizidi kuwa tete zaidi pale ambapo alipojiengua na kuanza kujitegemea huku bosi wake akijiuliza kwanini aliamua kufanya hivyo.
"Kipindi nilichokuwa nikifanya kazi na Jose, nilifanikiwa kujifunza mambo mengi sana na kunipa fursa ya kupiga hatua kubwa katika maisha yangu ya ukocha. Unajikuta unakuwa na mapenzi makubwa na yeye na kumfanya kuwa mfano wako. Nilitaka kuwa kama yeye, kujua kila alichokuwa anakijua na kufyonza kila kitu alichokuwa akinipa."
"Lakini sasa unapoangukia upande mwingine wa Mourinho ndipo utakapoona utofauti na kugundua kwamba kumbe ulikuwa unafanywa kipofu bila kujijua. Ana kila kipaji cha kupata kilicho bora kutoka kwako, kitu ambacho kina faida na hasara zake."
'Sasa kwa upande wangu matokeo yalikuja kama hivi ambavyo niliamua kujiengua na kuanza kusimama mwenyewe na kufundisha soka.'
Wakati Villas-Boas alipohama kutoka klabu ya Porto kwenda Chelsea mwaka 2011, ikiwa imepita miaka saba tangu Mourinho kufanya vivyo hivyo, ndipo pale alipoanza kufananishwa kwa kiasi kikubwa na Mourinho.
Lakini kitu kibaya kwake ni pale ambapo wakati mwenziwe Mourinho alifanikiwa kushinda makombe mawili ya Premier League kwenye kipindi chake cha mwanzo akiwa Stamford Bridge, Villas-Boas alijikuta akipata wakati mgumu kwenye maisha ya soka la England kabla ya kutupiwa virago mwaka uliofuata.
Villas-Boas anakiri kwamba alichukua uamuzi wa kuja England mapemo mno: "Kuikubali kazi ya kuwa meneja wa Chelsea ni uamuzi nilioufanya mapema sana na sikupaswa kufanya hivyo.
'Sikuwa na nimekuwa tayari kubeba jukumu lile. Nilikuwa naweza kufanya kile kinachopaswa kufanya na meneja, lakini sikuwa flexible katika njia zangu za ufundishaji. Wakati nikiwa Tottenham nilikuwa na utofauti kidogo."
'Katika soka la usindani unatakiwa kubadilika kila siku. Lengo kuu ni kuhakikisha kila mchezaji anachangia mafanikio ya timu na si mtu mmoja-mmoja. Kingine ukiwa kama kocha unatakiwa kuwa na namna tofauti-tofauti ya kuwasiliana na kila mchezaji, huwezi kuongea na kila mchezaji kwa namna moja, utafeli.'
'Wakati nikiwa Chelsea kufanya kazi kama kundi lilikuwa ni jambo muhimu sana, lakini mimi nilisimamia zaidi itikadi zangu.'
Kwa sasa Villas-Boas hafanyi kazi kwenye timu yoyote baada ya kuachana na klabu ya Zenit St Petersburg ya Russia mwishoni mwa msimu uliopita kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia na kuamua kurejea Portugal.

0 comments:
Post a Comment