Wednesday, October 5, 2016

Baada ya Toto kukufungwa 1-0 mchezo wa Jumapili dhidi ya Ndanda FC, kocha mkuu wa Toto Africans Rogasian Kaijage ametangaza kuachia ngazi nafasi ya kuifundisha timu hiyo ya jijini Mwanza.

“Ni kweli nimefanya uamuzi huo toka jana, leo ndiyo nilikuwa napeleka barua kwa uongozi ili kuwaambia rasmi. Jana nilitoa taarifa ya awali kwa message lakini ni kweli kwamba mimi nimeiacha Toto. Ni suala refu lakini kimsingi tanzania watu huwa tunafanya vitu bila kujua mwelekeo wake, katika mpira tuna tatizo la uchungu wa matokeo lakini si uchungu wa kuiandaa timu au kuandaa matokeo.”

“Naweza kusema nilikuwa najitolea kuwasaidia lakini kwasababu imetokea matokeo yamekuwa sio mazuri sasa uchungu wa matokeo kwa ambao hawajui matatizo yaliyomo ndio walitaka kunivamia jana na kutaka kunipiga wakisema niwaachie timu yao. Sasa kama nawasaidia halafu watu wanataka timu yao kwasababu ya matokeo kwanini nisiwaachie.”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video