Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea
kesho Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo
kati ya Young Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya
Morogoro ukipangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 6 kipendelea cha kwanza, Young Africans
wametambulisha Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa nyumbani kwa sasa baada ya
kuleta maombi Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) ambako baada ya
kuyafanyia tathimini kwa mujibu kanuni hiyo ya sita, kipendelea cha
sita, TFF imeiridhia klabu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, kutumia uwanja wa
Uhuru.
Hatua hiyo inafuatia na Serikali – mmiliki wa viwanja vya Uhuru na
Uwanja Mkuu wa Taifa, kuzuia klabu hiyo pamoja na ya Simba kutumia
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa michezo yao ya nyumbani kutokana na
vurugu.
Michezo mingine itakayopigwa Jumatano ni kati ya Mbeya City ya Mbeya
na Simba ya Dar es Salaam, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya; Majimaji itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Majimaji mjini Songea wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Tanzania
Prisons kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Stand United itaikaribisha Azam FC
kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na katika mkoa huo huo
Mwadui itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye dimba la Mwadui Complex
huku timu pinzani za Mwanza ‘Mwanza Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans
itapigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo. Alhamisi Oktoba 13, 2016
Ruvu Shooting itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mabatini.
0 comments:
Post a Comment