Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Hans Van Pluijm mapema leo asubuhi ametokea katika mazoezi ya timu kuwaaga rasmi wachezaji pamoja na wasaidizi wake wa benchi la ufundi .
Kuanzia sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Juma Mwambusi mpaka hapo klabu hiyo itakapomtangaza kocha mkuu mpya kurithi mikoba ya mholanzi huyo
.
Akitoa nasaha zake, Van Pluijm amewaasa wachezaji kuendelea kujituma na kufanikisha azma yao ya kueteta taji lao kwa mara nyingine, kudumisha nidhamu, kupendana na kutanguliza mbele masilahi ya timu kuliko masilahi binafsi.
Kwa niaba ya wenzake nahodha wa klabu hiyo Nadir Haroub alitoa neno la shukrani kwa kocha na kuahidi kuifanyia kazi rai yake na yote aliyokuwa akiwafundisha.
Van Pluijm amejiuzulu baada ya kufikiwa na taarifa za uijio wa kocha mpya Mzambia George Lwandamina ilhali wakati taratibu zote za kumleta zilifanyika bila kuarifiwa.
0 comments:
Post a Comment