Monday, October 17, 2016

Liverpool leo wanaikaribisha Manchester katika muendelezo wa michezo ya EPL, mchezo utakaofanyika kunako Uwanja wa Anfield saa nne kamili usiku wa leo.

Livepool wanaingia katika mchezo huu wakiwa na wasiwasi wa kutokuwa na nyota wao Adam Lallana na Georginio Wijnaldum kutokana na kuendelea kuuguza majeraha yao.

Mabeki Nathaniel Clyne na Dejan Lovren wamerudi na watakuwepo leo bila kusahau kiungo Mjerumani Emre Can.

Kwa upande wa Manchester United, kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan na beki  Luke Shaw wanarejea leo.

Phil Jones kwa upande wake hatakuwepo kwenye mchezo wa leo.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp: "Ukichana na msimao wa ligi ulivyo, huu ni mchezo muhimu sana kwetu. Najua vizuri kuhusu historia ya mchezo huu, napenda stori mbalimbali kuhusu huu mchezo, dunia nzima itakuwa ikiangalia mchezo huu, ni heshima kuwa kuwa sehemu ya tukio hili.

"Mwisho wa siku ni juu yetu kucheza kwa kiwango bora. Hatutakiwi kupuuzia kitu chochote kuhusu mchezo huu. Lazima tuwe na utayari mkubwa.

Manchester United ni timu yenye ubora wa hali ya juu na lazima tuwaheshimu, kama tunavyofanya. Lakini hii ni Anfield

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameelezea juu ya ushangiliaji usio wa heshima: "Kwenye soka kuna mambo mengi ambayo mengine yanaudhi na mengine yanafurahisha, sasa kuelekea mchezo huu tunapaswa kuwa makini na kupambana kwa hali zote."


MATCH FACTS
Head-to-head
  • Kipigo kwa Liverpool leo itakuwa ni mara ya kwanza kupoteza mechi tatu za ligi mfululizo dhidi ya Manchester United tangu Januari 2005.
  • United wameshinda mechi zao nne zilizopita zaligi dhidi ya Liverpool na saba kati ya tisa zilizopita.
  • Kipigo hicho cha mechi nne mfululizo kwa Liverpool ni matokeo mabaya zaidi tangu walivyopoteza mechi tano mfululizo kwa United March 2008.
  • Liverpool wamepoteza mechi 67 za ligi dhidi ya United, mechi nyingi zaidi dhidi ya timu nyingine yoyote pinzani.
  • Timu hizi mbili hazijawahi kutoka sare kwenye mechi za ndani tangu ilivyotokea mara ya mwisho Oktoba 2011 walivyotoka sare ta bao 1-1.
  • Steven Gerrard ambaye ana magoli nane ndiyo kinara wa ufungaji kati ya timu hizi mbili kwenye Premier League. Wayne Rooney na Robbie Fowler kila mmoja ana magoli sita.
  • Klopp amepoteza mchezo mmoja tu kati ya mitano aliyokutana na Jose Mourinho, akishinda michezo mitatu na kutoka sare mara moja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video