Hatimaye
kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mholanzi, Hans van der Pluijm amejiuzulu
kuifundisha klabu hiyo baada ya uongozi kuamua kubadili benchi la ufundi, huku
yeye mwenyewe akifichwa fichwa.
Pluijm
ameithibitishia Mshikemshike Viwanjani kuwa amefikia maamuzi hayo ya kuachana
na Yanga akiamini mlango mmoja ukifungwa mwingine unafunguliwa.
Klabu ya
Yanga kupitia akaunti yao rasmi ya mtandao wa kijamii wa Instagram
imethibitisha kujiuzulu kwa kocha huyo ambapo wameonesha kuthamini mchango
alioutoa kwa timu hiyo ya Jangwani.
Mabingwa hao
watetezi wameeleza kwa kirefu mafanikio aliyowapatia Pluijm katika kipindi
chote alichoifundisha Yanga ambapoo siku za karibuni aliifikisha timu hiyo
hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Africa.
Mbali na
hivyo, msimu uliopita, aliweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara na
Kombe la Azam Sports Federation Cup.
Taarifa za
uhakika zinaeleza kuwa Yanga imeamua kuvunja benchi nzima la ufundi na walimpa
ofa Pluijm ya kuwa Mkurugenziwa wa Ufundi, lakini amekataa.
Haya
yanakuja kutokana na uongozi wa Yanga kudaiwa kufikiwa makubaliano na na kocha
mkuu wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina ambaye yuko nchini toka jana na
taarifa za awali zinaeleza kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment