Friday, October 14, 2016

Na Hissan Salum Iddi.
MFUMO wa uchezaji wa Yanga SC miaka nenda rudi umekuwa ukitegemea krosi ili kuzalisha mabao, ndio maana mawinga bora wengi Tanzania wamepata kuichezea Yanga.
Geofrey Furaha Mwashiuya ni winga bora mwenye kusadifu sifa ya winga anayehitajika katika utamaduni wa mfumo wa Yanga SC.
 Uwezo wake wa kupiga chenga, kukimbia na mpira kwa kasi,umakini wa utoaji pasi,utulivu anapokuwa na mpira,uwezo wa kupiga mashuti miguu yote miwili, uwezo wa kukaa na mpira,kukaba kwa nguvu pale anapopoteza mpira,  upigaji krosi kwa usahihi zaidi umekuwa ukiisaidia Yanga kila anapopata nafasi ya kucheza. 
Kwa aina ya washambuliaji tulionao wenye njaa, wazoefu na wajanja wa kujiweka katika nafasi za kufunga, basi kupitia miguu ya Mwashiuya bila shaka tungenufaika zaidi.
Beki namba mbili Juma Abdul amekuwa msaada mkubwa katika umiminaji krosi zenye macho na madhara makubwa kwa mpinzani, hata hivyo hivi karibuni wapinzani wamemsoma na kumnyima nafasi ya kupanda mbele ili kuweza kupiga krosi. Je , nani anaweza kuwa suluhisho? bila shaka yoyote Geofrey Mwashiuya.
June 27 , 2015 Mwashiuya alicheza mchezo wake wa kwanza katika klabu Yanga ilikuwa dhidi ya SC Villa, mchezo ambao ulimtambulisha rasmi Mwashiuya katika ramani ya soka la Tanzania kama Lunyamila mpya, siku ambayo karibu kila mpenzi wa soka aliyepata kushuhudia pambano lile aliondoka na jina la Mwashiuya kichwani, huku wana- Yanga wakijinasibu kwa usajili huo.
Mwaka mmoja na miezi 4 imepita lakini kiwango cha Mwashiuya kimekuwa maji kupwa maji kujaa, huku tatizo la winga kariba ya Mwashiuya vikiikabili timu ya Yanga.
Yanga inahitaji mpiga krosi wa nyongeza kuliko kutegemea krosi za Juma Abdul tu, Mwashiuya sasa yupo fit baada ya kurejea katika majeraha,  ni jukumu la Hans Van Pluijm kuhakikisha kiwango cha Mwashiuya kinaimarika zaidi kwa kumpatia mafunzo bora zaidi, matunzo ya ukaribu na nafasi ya kucheza ili aweze kujiamini na kujisahihisha kwa kupata uzoefu kwani anaweza kuipatia matokeo bora zaidi klabu ya Yanga ukizingatia kijana huyu ndiye winga bora kwa sasa nchini na bado umri wake mdogo,  ndio kwanza ana miaka 19 tu.
Follow Instagram : hissansalum.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video