Saturday, October 15, 2016

Safari ya Simba kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulikosa kwa kipindi kirefu imezidi kuwa tamu baada ya kuifunga Kagera Sugar kutoka Kagera mabao 2-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa wenye msisimko wa aina yake, timu zote zilianza kwa utulivu mkubwa kwa kushambuliana kwa zamu, huku mara nyingi mpira ukichezwa eneo la kiungo.

Kagera Sugar ambao tangu msimu huu uanze wamekuwa na matokeo mengi chanya wakiwa chini ya kocha kijana Mecky Mexime, walicheza kwa nidhamu kubwa bila ya kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwao.

Wakicheza bila mshambulizi wao kutoka Burudi aliyeanzia bechi Laudit Mavugo, Simba walijikuta wakipata wakati mgumu kutoboa ukuta wa Kagera kutokana na safu yao ya ushambulizi iliyokuwa chini ya Fredrick Blagnon kubanwa vilivyo.

Hata hivyo mnamo dakika ya 43, Simba walipata bao lao la kwanza lililowekwa kimiani na kiungo wake Mzamiru Yassin aliyeunganisha kona mujarab ya kiungo mshambuliaji aliye kwenye ubora wa hali ya juu Shiza Kichuya.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili mpira na kasi ile ile kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na kucheza kwa tahadhari kubwa.

Dakika ya 76 Simba walipata bao la pili kupitia kwa Shiza Kichuya kufuatia kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Mohammed Ibrahim kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.

Dakika ya 90 Mavugo ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Blagnon almanusura aifungie Simba bao lakini mpira uligonga mwamba wa chini na kuokolewa na mabeki wa Kagera Sugar.

Matokeo ya leo yanazidi kuibakisha Simba kileleni kwa kuwa na jumla ya alama 23.

Matokeo ya mechi nyingine.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video