
Taarifa zilizoifikia Mpenja Sports hivi punde zinaeleza kuwa Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali, ameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na mwili wake kuokotwa maeneo ya Kimara na kupelekwa moja kwa moja Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuhifadhiwa ili kungoja taratibu zingine.
Kwa mujibu wa chanzo chetu inaelezwa kuwa ameuawa kwa kupigwa na vitu vizito na ndipo baadaye wasamaria wema kuukuta mwili wake na kuupeleka hospitali.
Taarifa zaidi zitazidi kuwajia.
0 comments:
Post a Comment