Friday, October 14, 2016

  BAADA ya kucheza mechi nane, Shiza Ramadhan Kichuya hadi sasa ndiye mshambuliaji hatari zaidi katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Kichuya ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, ameishapachika timu yake mabao sita na ndiye anaongoza msimamo wa wafungaji na kuwafunika kabisa washambuliaji wa kigeni.

Kichuya amewafunika wageni katika kikosi chake ukianza na Frederick Blagnon ambaye hana bao na Laudit Mavugo ambaye amefunga mabao matatu.

Kama hiyo haitoshi, Kichuya amewafunika washambuliaji wa kigeni pia katika timu nyingine ikiwemo Yanga ambayo ina Amissi Tambwe mfungaji bora wa msimu uliopita na Donald Ngoma.

Kichuya ambaye asili yake kiungo, ameisaidia Simba kushinda mechi sita katika ya nane ilizocheza za ligi hiyo.

Hata hivyo, inaonekana ushindani bado ni mbichi kabisa kwa kuwa washambuliaji hao wa kigeni hasa wale wa Yanga, wanaweza kuubadili mchezo wakati wowote.
Kichuya amefunga mabao matano kwenye mechi nne Mfululizo.
Alifunga goli moja kwenye mechi ya Ufunguzi wa VPL Agosti 20 Mwaka huu, Simba ikiichapa 3-1 Ndanda FC ya Mtwara.
Baada ya Hapo Simba ilitoka suluhu (0-0) na JKT Ruvu, halafu ikashinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Kichuya hakufunga.
 Kichuya akafunga bao la nne katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC.
 Baadaye Simba ikaichapa 2-0 Mtibwa Sugar, Kichuya hakufunga tena, lakini akaibuka Simba ilipoichapa 4-0 Majimaji FC ambapo alipiga mabao mawili, huku mengine yakifungwa na Jamal Mnyate.
Mechi ya watani wa Jadi, Yanga na Simba, Oktoba Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Kichuya aliisawazishia Simba kwenye sare ya 1-1.
Na Katikati ya wiki hii kule Mbeya, alipachika bao moja katika ushindi wa Simba wa 2-0 dhidi ya Mbeya City.
Kesho Simba itacheza na Kagera Sugar Uwanja wa Uhuru, Je, Kichuya atafanya nini?

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video