Thursday, October 6, 2016


KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inapenda kuufahamisha umma kuwa imemteua ndugu Abdul Mohamed kuwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, uteuzi ulioanza Oktoba Mosi mwaka huu.
Uteuzi huo ni sehemu ya mikakati ya Azam FC ya kuendesha timu kiueledi na tunaamini ujio wa Mohamed utaongeza nguvu kwenye eneo la uongozi na hatimaye kufikia malengo tuliyoyakusudia.
Azam FC inaamini katika uendeshaji mambo kiueledi ndani ya klabu na ndio maana imekuwa na safu ya uongozi iliyosheheni watu wenye taaluma mbalimbali.
Hivyo tunaamini kwa uzoefu aliokuwa nao Mohamed huko alikotoka akiwa kama mwandishi wa habari kwenye Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na nguvu kazi ya viongozi wengine utaweza kutufikisha kwenye mafanikio.
Majukumu ya kuendesha klabu kila siku yamekuwa na changamoto mpya zinazohitaji kutatuliwa kupitia nguvu kazi ya watu na Azam FC haitasita kuboresha mfumo wake wa uendeshaji wa klabu ili kuendana na changamoto hizo, kwa kuuongezea nguvu kazi pale inapohitajika ili kufikia mafanikio.
Mbali na kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye sekta ya habari akipita IPP Media, Clouds Media na BBC, Mohamed pia amesomea masuala ya Uhasibu na Fedha. Azam FC inamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya hayo katika ngazi ya soka.
img_0267
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba wakati akimtambulisha Abdul Mohamed kuwa Meneja mkuu wa Azam FC.

Imetolewa na Uongozi wa Azam F



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video